SIKILIZA MAKALA - KATIBA INAYOPENDEKEZWA - Mamlaka ya Wananchi, Utii na Hifadhi ya Katiba
SIKILIZA MAKALA
KATIBA INAYOPENDEKEZWA
Mamlaka ya Wananchi, Utii na Hifadhi ya Katiba
SIKILIZA MAKALA
KATIBA INAYOPENDEKEZWA
Mamlaka ya Wananchi, Utii na Hifadhi ya Katiba
Michuano ya soka ya CHAN kuwania ubingwa wa Afrika baina ya wachezaji wanaocheza soka nyumbani, intarajiwa kuanza Jumamosi ijayo tarehe 16 mwezi huu nchini Rwanda.
Mataifa 15 pamoja na Rwanda yatashiriki katika michuani hii inayitarajiwa kuwakusanya maelfu ya wapenzi wa soka katika nchi hiyo ya Afrika ya Kati.
Serikali ya Rwanda imetangaza kuwa hakutakuwa na malipo ya Visa kwa mashabiki wa mataifa yatakayoshiriki katika michuano hii watakaoamua kwenda nchini humo kuzishabikia timu zao.
#000000">Siku 30 baada ya Serikali ya Tanzania kuzuia matumizi ya picha ya kwanza ya Rais Magufuli, Hatimae picha imetolewa rasmi inayotakiwa kutumika kwenye ofisi za Serikali na zile za binafsi.
Nahodha wa timu ya taifa ya soka ya Cote D'voire na klabu ya Manchester City nchini Uingereza Yaya Toure amesema amesikitishwa sana kwa kukosa kuchaguliwa kuwa mchezaji bora wa soka barani Afrika mwaka 2015.
Toure mwenye umri wa miaka 32, alishinda taji hilo mara nne mfulilizo mwaka 2011, 2012, 2013 na 2014.
Toure ameongeza kuwa kutokana na juhudi zake kuisadia timu yake ya taifa kunyakua ubingwa wa Afrika na klabu yake, haikuwa rahisi kuamini kukosa tuzo hiyo na kuweka historia kuwa mchezaji aliyewahi kushinda tuzo hiyo mara tano.
Patrice Carteron ameondoka katika klabu ya soka ya TP Mazembe baada ya mkataba wake wa kuwa kocha kumalizika mwezi Desemba mwaka jana.
Uongozi wa klabu hiyo umetangaza rasmi kuwa umeachana na Carteron raia wa Ufaransa ambaye alijiunga na klabu hiyo yenye makao yake mjini Lubumbashi mwaka 2013 akitokea timu ya taifa ya Mali.
Kocha huyo atakumbukwa kuiongoza Mazembe kunyakua ubingwa wa klabu bora barani Afrika mwaka uliopita na kuisaidia klabu hiyo kufika katika fainali ya kombe la dunia baina ya vilabu nchini Japan mwezi Desemba mwaka jana.
Bakary Papa Gassama kutoka nchini Gambia, kwa mwaka wa pili mfululizo ameshinda tuzo ya refarii bora barani Afrika.
Gassama mwenye umri wa miaka 36 alikuwa refarii wa FIFA mwaka 2007 na mwaka 2012 alikuwa miongoni mwa marefarii walioshiriki katika michuano ya Olimpiki na hasa fainali kati ya Mexico na Brazil lakini kipindi hicho alikuwa afisa wanne katika mchuano huo.
Mwaka 2012 na 2013 alichezesha michuano ya mataifa bingwa barani Afrika pamoja na fainali za kombe la dunia mwaka 2014 nchini Brazil.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 07 Januari, 2016 amekutana na kufanya mazungumzo na Rais Mstaafu wa awamu ya tatu Mheshimiwa Benjamin William Mkapa na Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba Ikulu Jijini Dar es salaam.
Akizungumza mara baada ya Mazungumzo hayo Rais Mstaafu Mkapa amesema lengo la kukutana na Rais Magufuli ni kumpongeza kwa dhamana aliyopewa na watanzania kuiongoza nchi, kuunda serikali na kumtakia heri ya Mwaka Mpya.
Pierre-Emerick Aubameyang mshambuliaji wa timu ya taifa ya soka ya Gabon na klabu ya Borrussia Dortmund ya Ujerumani, ndio mchezaji bora wa mwaka 2015.
Aubameyang mwenye umri wa miaka 26 alipewa tuzo hiyo jijini Abuja jana usiku baada ya kupata alama 143 mbele ya mshambuliaji wa Manchester City na Cote Dvoire Yaya Toure aliyepata alama 136.
Andre Ayew, kutoka Ghana na anayechezea klabu ya Swansea nchini Uingereza, alikuwa wa tatu kwa alama 112.