Home » Node

CHAN 2016: Rwanda yaweka historia

Rwanda inaingia katika vitabu vya kihistoria kwa kuandaa mashindano makubwa ya soka barani Afrika kwa wachezaji wanaocheza nyumbani CHAN, kuanzia Jumamosi hii.

Hii ni mara ya kwanza kwa mashindano haya kufanyika nchini Rwanda na katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kat,i tangu kuzinduliwa kwake mwaka 2009 nchini Cote D'voire.

Kufungua Jengo la Wagonjwa wa Nje Mkoa wa Kaskazini Unguja

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,Ikulu na Utawala Bora Dkt.Mwinyihaji Makame kwa niaba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akifungua pazia kufungua Jengo la Wagonjwa wa Nje Hospitali ya Kivunge Wilaya ya Kaskazini A Mkoa wa Kaskazini Unguja,katika shamra shamra za Mapinduzi matukufu ya Zanzibar kutimia miaka 52 (wa pili kushoto) Naibu Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo Jecha,[Picha na Ikulu.]

Sherehe ya uzinduzi wa Taa za kuongozea Ndege Pemba

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akizungumza na wananchi katika sherehe za uzinduzi wa Taa za Kuongozea Ndege katika kiwanja cha ndege cha Pemba jana ikiwa ni katika shamra shamra za miaka 52 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar,(kulia) Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Mwanajuma Majid na (kushoto) Naibu Waziri wa Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano Issa Haji Ussi(GAVU)V

Messi aweka historia

Hatua ya Lionel Messi kunyakua taji la mchezaji bora katika mchezo wa soka duniani kwa mara ya tano na kuweka historia ya kuwa mchezaji wa kwanza kuwahi kufikia kiwango hicho, inaweka wazi mafanikio ya mshambuliaji huyu matata.

Messi mwenye umri wa miaka 28 raia wa Argentina, alianza kuichezea Barcelona mwaka 2001 akiwa kijana chipukizi na hadi sasa bado anakipiga na klabu hiyo.

CHAN 2016: Uchambuzi wa kundi B

Timu ya taifa ya soka ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo inayowajumuisha wachezaji wanaocheza soka nyumbani, Itaanza kuwani ubingwa wa michuano ya Afrika CHAN, dhidi ya Ethiopia siku ya Jumapili katika uwanja wa Huye mjini Butare.

Leopard imeshiriki katika makala yote ya CHAN tangu kuanzishwa kwake mwaka 2009 nchini Cote D'voire, mwaka ambao waliibuka mabingwa wa kwanza wa taji hili.

Pages

Ad
Subscribe to Focus Media RSS