Home » Node

Serikali ya Kenya inasema kuwa operesheni inaendelea nchini Somalia

Serikali ya Kenya inasema kuwa operesheni maalumu ya utafutaji na uokoaji inaendelea nchini Somalia siku chache tu baada wanamgambo wa Al-Shabab kutekeleza shambulizi la kushtukiza kwenye kambi moja ya wanajeshi wa Umoja wa Afrika na kudai kuwaua zaidi ya wanajeshi 100.

 

Kambi hiyo iliyoko kusino magharibi mwa nchi ya Somalia ilivamiwa na wanamgambo hao alfajiri ya siku ya Ijumaa, ikiwa ni shambulio jingine baya zaidi kutekelezwa na wanamgambo hao wakilenga kambi ya wanajeshi wa Umoja wa Afrika.

Rais wa Kenya, kuwaondoa watumishi wa Mungu waongo

Rais wa Kenya Uhuru Mwigai Kenyatta ameendelea kusisitiza azma ya Serikali ya kutaka kuwashughuikia na kuwaondoa watumishi wa Mungu waongo ambao wanatumia udhaifu wa raia kujilimbikizia mali kupitia sadaka.

Rais Kenyatta ameyasema haya akiwa mjini Mombasa, ambapo amewataka viongozi wa dini kushirikiana na Serikali katika kuwabaini wanaojiita watumishi wa Mungu lakini wamekuwa wakitumia mgogngo wa kanisa kujinufaisha.

Balozi Dkt. A. Mahiga,akutanana na wabunge wa A.Mashariki

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Dkt. Augustine Mahiga, (wanne kutoka kushoto), Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Dkt. Susan Kolimba, (watatu kutoka kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki, EALA, kutoka Tanzania, Mh. Shy-Rose Bhanji, 9wakwanza kushoto), Mh. Makongoro Nyerere (wapili kushoto), Mh. Angella Kizigha, (Wasita kutoka kushoto), naMh. Bernard Murunya).

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amekutana na Balozi wa Rwanda

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Rwanda nchini, Eugene Kayihura. Ambapo amemuahidi kuwa Tanzania itaendelea kushirikiana na Rwanda.

Akizungumza na Balozi  Kayihura  jana ,(jumatano 13, 2016) ofisini kwake, Magogoni jijini Dar es salaam, Waziri Mkuu amemshukuru  Balozi huyo kwa kumtembelea na ameahidi kuwa Serikali ya Tanzania itaendeleza ushirikiano ulipo baina ya nchi hizi mbili.

URA yashinda taji la Mapinduzi

Klabu ya soka ya URA ndio mabingwa wa taji la Mapinduzi Visiwani Zanzibar mwaka 2016.

URA iliishinda Mtibwa Sugar kutoka Tanzania bara kwa kuifunga mabao 3 kwa 1 katika fainali iliyochezwa Jumatano usiku katika uwanja wa Amman Visiwani Zanzibar.

Julius Ntambi alikuwa wa kwanza kuipa URA bao la ufunguzi katika kipindi cha kwanza cha mchuano huo, huku Peter Lwasa akifunga mabao mawili kipindi cha pili.

Bao la Mtibwa Sugar kuwafuta machozi lilitiwa kimyani na Jaffar Salum katika mchuano huo ambao Waganda waliutawala.

Pages

Ad
Subscribe to Focus Media RSS