Home » Node

Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) kushirikiana na Chuo Kikuu cha Komoro

Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) kimetiliana saini mkataba wa makubaliano juu ya mashirikiano na Chuo Kikuu cha Komoro mjini Moroni katika hafla maalum iliyofanyika tarehe 19 Januari, 2016 na kuhudhuriwa na uongozi wote wa Chuo Kikuu cha Komoro, Balozi wa Komoro nchini Tanzania Dkt. Ahmada El Badaoui Mohamed na Mwakilishi wa Balozi wa Tanzania nchini Komoro, Bw Mudrik Ramadhan Soragha.

Balozi Seif Ali Idd amemhakikishia Rais Dkt. John Pombe Magufuli kuwa hali ya Zanzibar ni shwari

Makamu wa Pili wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mheshimiwa Balozi Seif Ali Idd amemhakikishia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kuwa hali ya Zanzibar ni shwari na Wazanzibari wanasubiri kutangaziwa tarehe ya kufanyika kwa uchaguzi.

Balozi Seif Ali Idd ameyasema hayo Ikulu jijini Dar es salaam leo tarehe 20 Januari, 2016 mara baada ya kukutana na kufanya mazungumzo na Rais Magufuli.

Rais Magufuli amemuelezea Marehemu Asha Bakari Makame kuwa alikuwa Kiongozi Hodari

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemtumia salamu za rambirambi Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kufuatia kifo cha Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake Tanzania (UWT) Bi. Asha Bakari Makame kilichotokea jana tarehe 19 Januari, 2016 huko Dubai.

Pages

Ad
Subscribe to Focus Media RSS