Home » Node

Rais Magufuli akutana na kufanya Mazungumzo na Rais Mstaafu Kikwete

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete Ikulu Jijini Dar es salaam.

Katika Mazungumzo hayo Rais Mstaafu Kikwete amemtakia Rais Magufuli heri ya Mwaka mpya na kumpongeza kwa uongozi mzuri.

Rais Kikwete pia amesema anaunga mkono juhudi mbalimbali zinazofanywa na Rais Magufuli ikiwemo ukusanyaji wa mapato ya serikali.

KATIBA INAYOPENDEKEZWA - UTANGULIZI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete alianzisha mchakato wa uandikaji wa Katiba Mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 2011 kutokana na maombi ya wananchi wakiwemo viongozi wa vyama vya Siasa walioonyesha uhitaji wa Katiba mpya inayoendana na mazingira ya sasa ya nchi yetu.

Mchakato huu umekamilika na kwa mujibu wa Sheria ya Kura ya Maoni ya mwaka 2013, taifa linasubiri kupiga kura ya maoni hapo Aprili 30, 2015 ya kufanya uamuzi wa kuikubali au kuikataa Katiba Inayopendekezwa.

Barack Obama kuchukua hatua kuhusu udhibiti wa silaha

Rais wa Marekani, Barack Obama hii leo anatarajiwa kutumia madaraka yake ya juu kuchukua hatua kuhusu udhibiti wa silaha, akiacha kutumia bunge la Congress, hatua inayoashiria kuwa uchaguzi wa mwaka huu utakuwa mgumu kwa chama chake.

Mwaka uliopita rais Obama alionesha waziwazi kitofautiana na wanasiasa wanaopinga mapendekezo yake, ambapo aliahidi kutumia madaraka ya rais, hatua inayopuuzilia mbali upinzani wa bunge la Congreaa dhidi ya mapendekezo yake.

Nchi ya Marekani imetangaza kuwa hivi karibuni itafunga rasmi kituo chake cha kijeshi

Nchi ya Marekani imetangaza kuwa hivi karibuni itafunga rasmi kituo chake cha kijeshi cha operesheni za ndege zisizo na rubani, kilichoko kusini mwa nchi ya Ethiopia.

Kituo hicho ambacho kipo umbali wa kilometa 400 kusini mwa mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa, kimekuwa kikitumika toka mwaka 2011, kutekeleza mashambulizi dhidi ya wapiganaji wa kijihadi kwenye pwani ya Afrika Mashariki.

Obama asema huwa hapaki nywele zake rangi

Rais wa Marekani Barack Obama amesema yeye huwa hapaki rangi nyele zake kuficha mvi kama viongozi wengine duniani.

Kiongozi huyo wa umri wa miaka 54 alikuwa akimjibu mwanafunzi mmoja kutoka Cambodia aliyekuwa amemuomba ushauri wa busara.

Bw Obama aliingia mamlakani 2009 akiwa na nywele nyeusi lakini miaka ilivyosonga ameanza kuwa na mvi nyingi.

Rangi ya nywele za rais huwa suala tata wakati mwingine, na viongozi wengi wamekuwa wakificha ukweli kwamba hupaka rangi nywele zao.

Waziri mashuhuri Kenya Anne Waiguru ajiuzulu

Waziri mwenye ushawishi mkubwa katika serikali ya Rais Uhuru Kenyatta amejiuzulu wadhifa wake baada ya shinikizo kutolewa ajiuzulu kutokana na tuhuma za ufisadi.

Bi Anne Waiguru, ambaye amekuwa Waziri wa Mipango na Ugatuzi, ameambia wanahabari Nairobi kwamba ameshauriwa na daktari wake “achukue muda kupumzika”.

Amewaambia wanahabari kwamba amemwandikia Rais Kenyatta akimtaka amuondolee majukumu yake.

Hata hivyo amesisitiza kwamba hana hatia.

Pages

Ad
Subscribe to Focus Media RSS