Home » Node

Rais Dkt. John Pombe Magufuli ameanza ziara ya siku nne

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 29 Julai, 2016 ameanza ziara ya siku nne katika mikoa ya Singida, Tabora, Shinyanga na Geita akitokea mkoani Dodoma, ambapo amezungumza na wananchi kwa lengo la kuwashukuru kwa kumpigia kura katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana na kueleza juhudi zinazofanywa na serikali katika kutatua kero za wananchi na kuwaletea maendeleo.

Bodi ya mikopo itakuwa wazi Julai 30, 2016 na Jumapili, Julai 31

Bodi ya Mikopo inapenda kuwataarifu wadaiwa wote waliopo Dar es Salaam kuwa Ofisi za Bodi zitakuwa wazi kwa siku mbili za kesho, Jumamosi, Julai 30, 2016 na Jumapili, Julai 31, 2016 kuanzia saa 3:00 asubuhi hadi saa 9:00 mchana ili kutoa huduma mbalimbali ikiwemo kuwasiliza wadaiwa.

 

Hii ni fursa muhimu kwa wadaiwa wote wa mikopo ya elimu ya juu ambao hawajaanza kulipa mikopo kupata taarifa kuhusu madeni yao.

 

Rais Magufuli amemteua Bw. Joseph Odo Haule kuwa Mwenyekiti mpya wa Bodi ya Mfuko wa Barabara.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ametengua uteuzi wa Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Barabara (Road Fund Board) Dkt. James Munanka Wanyancha.

Taarifa ya Katibu Mkuu Kiongozi iliyotolewa leo Mjini Dodoma imeeleza kuwa Rais Magufuli ametengua uteuzi huo kuanzia leo tarehe 28 Julai, 2016.

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameitaka Halmashauri ya wilaya ya Temeke kutoa ajira

WAZIRI MKUU ATOA SIKU MOJA KWA HALMASHAURI YA WILAYA TEMEKE  KUMALIZA TATIZO LA AJIRA ZA MIKATABA

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameitaka Halmashauri ya wilaya ya Temeke kuondoa wafanyakazi wa mkataba kwa  kuwapa ajira ya kudumu ifikapo Julai 30 mwaka huu.

Amesema kitendo cha kutowaajiri na kuwatumikisha kwa mikataba kwa muda mrefu kinasababisha wakose stahiki zao jambo ambalo si halikubaliki.

Pages

Ad
Subscribe to Focus Media RSS