Home » Node

Rais Magufuli, amemteua Mwenyekiti wa (ATCL)

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, amemteua Mhandisi Emmanuel Korosso kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL).

Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, imeeleza kuwa uteuzi wa Mhandisi Emmanuel Korosso unaanza mara moja.

Mhandisi Emmanuel Korosso anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Salim Msoma ambaye alimaliza muda wake.

 

Usalama umeimarishwa kwenye mji wa Mombasa nchini Kenya

Usalama umeimarishwa kwenye mji wa Mombasa nchini Kenya, baada ya kuuawa kwa wanawake watatu waliotekeleza shambulio la kigaidi dhidi ya Polisi wa kituo kikuu cha pwani ya Kenya.

Polisi mjini Mombasa wamesema kuwa wanawake waliohusika kwenye shambulio la kisu na bomu la kutengeneza kwa mkono, walikuwa ni raia wa Kenya na kwamba mmoja kati yao alikuwa amevalia mkanda wa mabomu ambao hata hivyo haukulipuka.

Makamu wa Rais Mh. Samia Suluhu Hassan amewasili mjini Mbabane - Swaziland leo kwa ajili ya kuhudhuria mkutano wa 36 wa SADC

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewasili mjini Mbabane - Swaziland leo kwa ajili ya kuhudhuria mkutano wa 36 wa Wakuu wa nchi na serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika- SADC. 
 
Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan atamwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika mkutano huo ambao utafanyika tarehe 29 Agosti  2016 ambapo Tanzania inatarajiwa kukabidhiwa nafasi ya Uenyekiti wa Jumuiya hiyo.

Pages

Ad
Subscribe to Focus Media RSS