Askari jela miaka 15 kwa kosa la kumuua bila kukusudia Daudi Mwangosi
Mahakama Kuu mjini Iringa nchini Tanzania imemhukumu jela miaka 15 askari wa kikosi cha kuzia ghasia Picifius Simon kwa kosa la kumuua bila kukusudia mwanahabari wa Daudi Mwangosi mwaka 2012.
Mwanahabari huyo alipoteza maisha wakati polisi walitumia nguvu kuwasambaratisha wafausi wa chama cha upinzani CHADEMA Wilayani Mufindi.













