Home » Node

UNMISS, imeguswa na ripoti za matukio ya “ubakaji”

Tume ya umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini, UNMISS, inasema imeguswa na ripoti za matukio ya “ubakaji”, yanayodaiwa kutekelezwa na wanajeshi wa Serikali na kwamba tuhuma hizo zimeanza kuchunguzwa.

Kwa mujibu wa UNMISS, inasema kuwa, idadi ya raia, wengi wakiwa ni wasichana wadogo, wamekuwa wakishambuliwa jirani na jumba la umoja wa Mataifa pamoja na maeneo mengine jirani kwenye jiji la Juba.

Adhabu kali ya kifungo gerezani kwa mtu yeyote atakaye oa mtoto

Nchi ya Gambia juma hili, imepitisha sheria inayokataza ndoa za utotoni na kutangaza adhabu kali ya kifungo gerezani kwa mtu yeyote atakaye kiuka sheria hii.

Chini ya sheria hii mpya, mwanaume atakae oa msichana wa chini ya umri wa miaka 18, atakabiliwa na kifungo cha miaka 20 jela, ambapo wazazi wake watahukumiwa kifungo cha miaka 21 jela, huku imam atakayebainika kufungisha ndoa hiyo atahukumiwa kifungo kama hicho.

Uchunguzi wa shambulio lillo igharimu maisha ya wanajeshi 17 mali

Maafisa wa usalama nchini Mali wamesema, uchunguzi zaidi unaendelea kufanywa katika mji wa Nampala, kubaini wahusika wa shambulio la hivi karibuni dhidi ya kambi ya jeshi la serikali iliyoko mjini humo, na ambalo liligharimu maisha ya wanajeshi 17 wa serikali.

Kwa upande wake Rais wa Mali Ibrahim Boubakar Keita, amesema serikali yake itafanya kila linalowezekana kuhakikisha shambulio kama hilo halitiokei tena.

Dkt.Winnie Mpanju-Shumbusho kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Benjamini Mkapa - Dodoma.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Dkt.Winnie Mpanju-Shumbusho kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Benjamini Mkapa - Dodoma.

Kabla ya Uteuzi huo, Dkt. Winnie Mpanju-Shumbusho alikuwa Mkurugenzi Mkuu Msaidizi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) lenye makao yake makuu Mjini Geneva nchini Uswisi na alimaliza mkataba wake tangu Mwezi Desemba 2015.

Uteuzi wa Dkt. Winnie Mpanju-Shumbusho umeanza leo tarehe 18 Julai, 2016.

Marekebisho madogo katika majina yaliyopo kwenye orodha ya wakurugenzi

Tunapenda kufanya marekebisho madogo katika majina yaliyopo kwenye orodha ya wakurugenzi wa Halmashauri za Majiji, Manispaa, Miji na Wilaya ambapo

- Dkt. Leonard Moses Massale ametangazwa kuwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma.

Jina hilo limeingizwa katika Orodha ya Wakurugenzi wa halmashauri kwa makosa, na kwa sababu hiyo Dkt. Leonard Moses Massale anaendelea kuwa Mkuu wa wilaya ya Ilemela Mkoani Mwanza.

Rais Dkt. Magufuli leo tarehe 07 Julai, 2016 amefanya uteuzi wa wakurugenzi wa halmashauri za majiji 5, Manispaa 21, Miji 22 na Wilaya (DC) 137 za Tanzania Bara.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 07 Julai, 2016 amefanya uteuzi wa wakurugenzi wa halmashauri za majiji 5, Manispaa 21, Miji 22 na Wilaya (DC) 137 za Tanzania Bara.

Uteuzi huo umetangazwa na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhandisi Mussa Iyombe ambapo kati ya wakurugenzi wote 185 walioteuliwa, 65 wameteuliwa kutoka orodha ya wakurugenzi wa zamani na 120 ni wakurugenzi wapya.

Rais Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Bw. Deogratius John Ndejembi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mkoani Dodoma.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 07 Julai, 2016 amemteua Bw. Deogratius John Ndejembi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mkoani Dodoma.

Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi amesema Bw. Deogratius John Ndejembi anachukua nafasi iliyoachwa na aliyeteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Bw. John Ernest Palingo ambaye amehamishiwa Wilaya ya Mbozi katika Mkoa wa Songwe.

Pages

Ad
Subscribe to Focus Media RSS