Rais Magufuli ihutubia Baraza la Eid el-Fitr
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amempongeza Mufti wa Tanzania Sheikh Aboubakar Zubeir bin Ali kwa juhudi zake za kuwaunganisha waislamu wote na kupanua uwigo wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) kutoa huduma za kijamii na ameahidi kuwa serikali ya awamu ya tano itaunga mkono juhudi hizo.























