Home » Node

Rais Dkt. John Pombe Magufuli amewaondoa hofu wafanyakazi

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amesema serikali imeamua kusimamisha kwa muda mfupi usiozidi miezi miwili zoezi la utoaji ajira mpya na upandishaji wa vyeo kwa watumishi wa umma kwa lengo la kupisha uhakiki wa watumishi wa umma katika orodha ya malipo ya mshahara na kuondoa watumishi hewa.

Rais Magufuli amesema hayo katika Jubilei ya miaka 50 ya Benki Kuu ya Tanzania (BOT) iliyofanyika katika ukumbi wa Benki hiyo, Mtaa wa Mirambo Jijini Dar es salaam.

Baada ya kulipa kodi, Kiwanda cha DANGOTE kimeruhusiwa kuingiza Makaa ya mawe na Gypsum

Wizara ya Nishati na Madini imeipatia kampuni ya Saruji ya Dangote mkoani Mtwara vibali kuruhusu meli mbili zinazoingiza makaa ya mawe na gypsum kupakua ili zitumike kiwandani hapo baada ya kukamilisha utaratibu wa kuzilipia kodi ya ongezeko la thamani (VAT) ya zaidi ya shilingi Bilioni mbili.

Pesa hizi na pamoja na malimbikizo ya malipo ya Ongezeko la thamani (VAT) ya makaa ya mawe  yaliyoingia mwezi wa kumi na moja mwaka jana (2015)

Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete kukabidhi kijiti Julai 23

Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akiongoza Kikao cha Kamati Kuu ya CCM, leo katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, mtaa wa Lumumba jijini Dar es Salaam, pamoja na mambo mengine, Kikao hicho kimejadii na kupitisha kuwa Mkutano Mkuu Maalum wa CCM utafanyika Julai 23, 2016, ambapo mkutano huo unatarajiwa kumchagua Rais Dk. John Magufuli kuwa Mwenyekiti mpya Taifa. Kulia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Philip Mangula na Kulia ni Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana.

Pages

Ad
Subscribe to Focus Media RSS