Home » Node

Vongozi mbalimbali duniani wanaedelea kutuma risala za rambirambi baada ya kuuawa kwa Mbunge wa chama cha Leba Jo Cox

Vongozi mbalimbali duniani wanaedelea kutuma risala za rambirambi baada ya kuuawa kwa Mbunge wa chama cha Leba Jo Cox hapo jana aliyepigwa risasi na kudungwa kisu.

Mbunge huyo mwenye umri wa miaka 41, alishambuliwa wakati alipokuwa katika eneo bunge lake na mwanamume ambaye tayari ameshakamatwa na inadaiwa kuwa alimtamka neno Uingereza kwanza kabla ya kutekeleza shambulizi hiyo.

TCRA Yazima IMEI zaidi ya 600,000

Mamlaka ya Mawasiliano nchini Tanzania imeanza zoezi la kuzuia mawasilino ya simu za mkononi ambazo ni bandia.

Mamlaka hayo yanasema tayari mawasiliano katika simu zaidi ya Laki 6, yamezuiwa zoezi ambalo limesabisha changamoto za mawasilian kwa wamiliki wa simu hizo.

Tanzania inajiunga na Cameroon, Afrika Kusini na Nigeria kuungia simu hizo ambazo watalaam wa afya wanasema zina madhara makubwa lakini pia kwa sababu za kiusalama.

Madaktari wasiokuwa na mipaka ya MSF, wametangaza kutochukua fedha zozote kutoka kwa Umoja wa Ulaya.

Madaktari wasiokuwa na mipaka ya MSF, wametangaza kutochukua fedha zozote kutoka kwa Umoja wa Ulaya.

Shirika la Madaktari hao wamesema sababu yao ya kuchukua uamuzi huo ni kwa sababu ya sera mpya ya Umoja huo kuhusu wakimbizi.

MSF inasema, mkataba wake na Uturuki kuwa nchi hiyo iwachukue wakimbizi wote watkaofikia Ugiriki haukubaliki.

Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete Balozi wa Heshima (Goodwill Ambassador) wa Maendeleo ya Kilimo

MJUMBE wa Bodi ya Kituo cha Ufundi cha Kilimo na Maendeleo Vijijini (Technical Centre for Agricultural and Rural Cooperation, CTA) chenye makao makuu mjini Wageningen, Uholanzi, Prof. Faustin Kamuzora, akikabidhi kwa Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete uteuzi wa kuwa Balozi wa Heshima (Goodwill Ambassador) wa Maendeleo ya Kilimo katika Mabara ya Afrika, Karibiani na Pasafiki, uliofanywa na Kituo hicho cha CTA, Pfrof. Kamuzora aliwasilisha uteuzi huo, alipokwenda Ofisini kwa Dk.

Mashirika ya kiraia nchini Burundi, yanasema hawana imani na mratibu wa mazungumzo ya amani nchini humo

Mashirika ya kiraia nchini Burundi, yanasema hawana imani na mratibu wa mazungumzo ya amani nchini humo rais wa zamani wa Tanzania, Benjamin Mkapa.

Wanaharakati hao wanaotetea watu wanaoishi na virusi vya Ukimwi, wanasema uamuzi wao unakuja baada ya mratibu huo kukutana na muungano wa vyama vya upinzani CNARED jijini Brussels nchini Ubelgiji.

Wanakosoa hatua ya Mkapa kukutana na wapinzani hao kwa madai kuwa wao ndio chanzo cha ukosefu wa amani nchini mwao.

 

Miili ya wahamiaji 34 ilitupwa na walanguzi wa biashara haramu ya binadamu imepatikana

Miili ya wahamiaji 34 ikiwemo ya watoto 20, ambayo ilitupwa na walanguzi wa biashara haramu ya binadamu imepatikana katika Jangwa moja nchini Niger.

Ripoti zinasema kabla ya watu hao kupoteza maisha walikuwa safarini kwenda kutafuta hifadhi katika nchi jirani ya Algeria.

Kupatikana kwa miiili ya watu hao kumethibitishwa na Wizara ya Mambo ya ndani nchini Niger.

Watu 400 wameuawa nchini Ethiopia

Shirika la Kimataifa la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch linasema tangu mwezi Novemba mwaka uliopita, watu 400 wameuawa nchini Ethiopia.

Amnesty International inasema watu hao wameuawa mikononi mwa maafisa wa usalama nchini humo kwa kujaribu kuikosoa serikali ya Addis Ababa.

Hata hivyo, serikali imetupilia mbali ripoti hiyo na kusema haina ukweli wowote.

Pages

Ad
Subscribe to Focus Media RSS