Wakuu wa mikoa na wilaya watakiwa kutoa taarifa ya upungufu wa vitanda hospitalini
Waziri wa maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto UMMY MWALIMU, amewaagiza wakuu wa mikoa na wilaya kote nchini kutoa taarifa ya upungufu wa vitanda katika hospitali za serikali zilizopo katika maeneo yao ili serikali iendelee kuboresha huduma za afya
Waziri MWALIMU ametoa aagizo hilo katika hospitali ya Taifa Muhimbili jijini DSM, wakati kipokea vitanda na magodoro vyenye thamani ya Shilingi Milioni 88.7 kwa ajili ya wodi mpya ya wazazi kufuatia agizo la Rais Dkt. JOHN MAGUFULI.














