IMETIMIA; Ahadi ya bilioni 12.3 aliyotoa Rais Magufuli siku ya Mahakama
Wizara ya Fedha na Mipango imetoa sh.bilioni 12.3 kwa ajili shughuli za mahakama ikiwa ni sehemu ya ahadi ya Rais Dk. John Pombe Magufuli aliyoiahidi katika kilele cha maadhimisho ya siku ya mahakama.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango amesema fedha hiyo imetolewa kwa kutimiza ahadi ya Rais ya uendeshaji wa shughuli za mahakama.
"Sherry Party"
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga akihutubia wakati akimuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli katika Mchapalo wa Mwaka Mpya kwa Mabalozi na Wawakilishi wa Taasisi mbalimbali za Kimtaifa maarufu kama "Sherry Party" Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumatatu February 8, 2016
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akimjulia hali Mufti Mkuu wa Tanzania
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa kuitisha kikao cha viongozi wa dini zote
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema ataitisha kikao cha viongozi wa dini zote hivi karibuni ili wapange na kuainisha ni mambo gani ambayo wanaweza kutoa ushauri kwa Serikali na kupata njia bora ya kuwahudumia Watanzania.
Ametoa ahadi hiyo leo mchana (Jumapili, Februari 7, 2016) wakati akizungumza na mamia ya waumini walioshiriki ibada ya kumsimika Askofu Mkuu wa Pili wa Kanisa la Evangelistic Assemblies of God Tanzania (EAGT), Askofu Dk. Brown Abel Mwakipesile iliyofanyika kwenye kanisa la EAGT la Mlimwa West nje kidogo ya mji wa Dodoma.
Chad kuridhia itifaki iliyoanzisha Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu
Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu (AfCHPR) imeendelea kuongeza wanachama baada ya nchi ya Chad kuridhia itifaki iliyoanzisha Mahakama hiyo yenye makao yake makuu jijini Arusha.
Hatua hiyo inafanya Chad kuwa nchi ya 30 kuridhia itifaki hiyo kati ya nchi 54 wanachama wa Umoja wa Afrika (AU).
Hata hivyo, kati ya nchi hizo 30, ni nchi 7 tu ndizo zilizotoa tamko la kukubali mamlaka ya Mahakama ya Afrika kuweza kupokea kesi za watu binafsi na mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs) kwa mujibu wa kifungu cha 34(6).
Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akiongoza kikao cha Kamati Ku Maalum ya CCM
Hotuba Rais Magufuli kwenye Maadhimisho ya miaka 39 ya CCM
Kuzaliwa kwa CCM
Katika Mkutano Mkuu wa Pamoja wa TANU na ASP uliofanyika tarehe 22 Septemba, 1975 Rais wa TANU, Mwalimu Nyerere alisisitiza kwamba Tanzania ni nchi yenye Chama kimoja;
“Lakini kwa sababu kuna vyama viwili TANU na ASP, Katiba inazungumza juu ya Chama kimoja, hicho Chama kimoja kwa kweli ni vyama viwili … Siasa ya TANU na ASP ni moja yaani Ujamaa na Kujitegemea. Midhali Katiba ya Tanzania ni ya Chama kimoja, Katiba hiyo inataka hicho Chama chenye Siasa ya Ujamaa na Kujitegemea kishike hatamu na uongozi wa nchi”. (Tathmini ya Miaka 20 ya CCM, uk. 3-4).
Hotuba ya Rais Mstaafu Kikwete kwenye Maadhimisho ya miaka 39 ya CCM
Kuzaliwa kwa CCM
Katika Mkutano Mkuu wa Pamoja wa TANU na ASP uliofanyika tarehe 22 Septemba, 1975 Rais wa TANU, Mwalimu Nyerere alisisitiza kwamba Tanzania ni nchi yenye Chama kimoja;
“Lakini kwa sababu kuna vyama viwili TANU na ASP, Katiba inazungumza juu ya Chama kimoja, hicho Chama kimoja kwa kweli ni vyama viwili … Siasa ya TANU na ASP ni moja yaani Ujamaa na Kujitegemea. Midhali Katiba ya Tanzania ni ya Chama kimoja, Katiba hiyo inataka hicho Chama chenye Siasa ya Ujamaa na Kujitegemea kishike hatamu na uongozi wa nchi”. (Tathmini ya Miaka 20 ya CCM, uk. 3-4).
Kilele cha maadhimisho ya miaka 39 ya kuzaliwa CCM
HISTORIA YA CCM TANGU TANU NA ASP
Chama cha Mapinduzi (CCM) kilizaliwa tarehe 5 Februari, 1977 kutokana na kuvunjwa kwa vyama vya Tanganyika African National Union (TANU) na Afro-Shirazi Party (ASP).




















