Waziri mkuu Matteo Renzi ameionya nchi ya Misri
Wakati Serikali ya Italia ikimzika raia wake Giulio Regeni, waziri mkuu Matteo Renzi ameionya nchi ya Misri na kusema kuwa urafiki wao uko mashakani kutokana na uchunguzi wao kushindwa kueleza ni namna gani raia wake aliuawa.
Waziri mkuu Renzi amesema Serikali ya Misri ilitoa ushirikiano kwenye madai yake kwamba wachunguzi wa nchi yake wahusishwe kufanya uchunguzu kuhusu kifo cha Regen ambaye mwili wake ulipatikana ukiwa na majeraha yanayoenesha ishara kuwa aliteswa kabla ya kuuawa.
Watungua 'chopa' wanne wafungwa miaka 60
Raia wanne wa Tanzania waliokuwa wanakabiliwa na kesi ya mauji ya mwanamazingira raia wa Unigereza ambaye helcopter yake ilidunguliwa, wamehukumiwa kifungo cha miaka 20 jela kwa kosa la kumiliki silaha za moto kinyume cha sheria.
Licha ya watuhumiwa hao kutokiri kuhusika na mauji ya rubani huyo, iwapo watapatikana na hatia ya kosa la kuu, huenda wakahukumiwa kunyongwa kwa mujibu wa sheria za Tanzania, ambapo hata hivyo haijatekeleza kwa muda mrefu adhabu hiyo.
Wapiganaji makundi ya kiislamu wameshambulia kambi nchi ya Mali
Wapiganaji wanaodaiwa kuwa ni kutoka makundi ya kiislamu wameshambulia kambi ya wanajeshi wa kulinda amani wa umoja wa mataifa kaskazini mwa nchi ya Mali kwenye mji wa Kidal, ambapo watu kadhaa wameripotiwa kufa na wengine kujeruhiwa, amesema msemaji wa kundi la vuguvugu la Azawadi.
Kurejeshwa nchini Burundi, maofisa watatu wa jeshi
Nyaraka za siri zilzizopatikana, zimeonesha kuwa mkuu wa tume ya walinda amani nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, ameagiza kurejeshwa nchini Burundi, maofisa watatu wa jeshi la nchi hiyo kwa tuhuma za kuhusika na vitendo vya ukiukaji wa haki za binadamu.
AJALI : Basi la Simba Mtoto - Watu 11 Wafariki Dunia
Ajali mbaya ya barabarani imetokea mkoani Tanga leo asubuhi wakati Basi la Kampuni ya Simba Mtoto ya Tanga lilipogongana na Lori uso kwa uso katika eneo la Pangamlima Wilayani Korogwe mkoani humo.
Taarifa za awali kutoka eneo la tukieo zinaeleza kuwa watu 10 wanahofiwa kupoteza maisha na wengine kujeruhiwa vibaya atika ajali hiyo.
Roboti ya Mende kuokoa wahanga wa maporomoko
Wanasayansi nchini Marekani wametengeneza roboti inayofanana na mende ambayo inaweza kutumiwa kuwaokoa watu kunapotokea tetemeko la ardhi.
Watafiti wanasema roboti hiyo inatumia mbinu zinazotumiwa na mende kutembea kwenye nyufa kupenya vifusi na kuwaokoa walionaswa katika maporomoko.
Wanasayansi hao wanasema kuwa endapo roboti hiyo inawezavishwa kamera kisha ikatumwa kwenye vifusi vya jengo lililoporomoka inaweza kurahisisha uchunguzi wa usalama wa vifusi kabla ya makundi waokoaji kuingia.
Ukubwa wa roboti hiyo ni sawa na kiganja cha mwanadamu.
Aliyeishi muda mrefu na moyo wa kupandikizwa afariki
Bw McCafferty alipatikana na maradhi ya moyo akiwa na umri wa miaka 39.
Alifanyiwa upasuaji na Sir Magdi Yacoub.
Upasuaji wa kwanza wa kupandikiza moyo uliofanikiwa ulifanyiwa nchini Afrika Kusini mwaka 1967 na Prof Christiaan Neethling Barnard na kundi la matabibu 30 katika hospitali ya Groote Schuur, Cape Town.
Mgonjwa wao, Louis Washkansky, alifariki siku 18 baada ya kupokea moyo mpya.
Mwanamume aliyeishi muda mrefu duniani na moyo wa kupandikizwa amefariki, baada ya kuishi miaka 33 na moyo huo.
Licha ya kwamba Syria imegubikwa na vita, Maisha yanaendelea
Wanandoa Hassan Youssef na Nada Merhi wakipigwa picha mbele ya majengo yaliyoharibiwa na vita.
Wachezaji wa timu ya Leopards wa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo wamepewa zawadi ya magari
Wachezaji wa timu ya Leopards wa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo wamepewa zawadi ya magari aina ya Prado baada ya kutwaa ushindi wa ubingwa wa Afrika CHAN, kwenye mashindano yaliofanyika nchini Rwanda.






























