Home » Node

Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete mwakilishi usuluhishi Libya.

Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ameteuliwa na Mheshimiwa  Dkt. Nkosazana Dlamini Zuma, Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika kuwa Mwakilishi wa Umoja wa Afrika  katika mchakato wa usuluhishi wa mgogoro wa Libya.

Kufuatia uteuzi huo uliotangazwa rasmi na AU jana katika Kikao cha Wakuu wa Nchi za Afrika, Rais Mstaafu Kikwete leo asubuhi amekutana na Dkt. Zuma makao makuu ya AU leo na kufanya nae mazungumzo kuhusu jukumu alilokabidhiwa.

Rais Magufuli amhamisha Naibu Katibu Mkuu Sheria na Katiba

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemhamisha Bi. Suzan Paul Mlawi aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, kwenda kuwa Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Manejimenti ya utumishi wa umma na Utawala Bora.

Taarifa ya Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue, imeeleza kuwa uhamisho huo umeanzia tarehe 26 Januari, 2016.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa pamoja na shughuli nyingine za Unaibu Katibu Mkuu, Bi. Suzan Paul Mlawi, atashughulikia eneo la Utawala Bora.

Rais Dkt. John Pombe Magufuli akutana na Jaji Damian Lubuva

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amelaani kitendo cha watu wanaosadikiwa kuwa ni majangili kumuua kwa kumpiga risasi Rubani wa helkopta Kepteni Roger Gower, raia wa Uingereza na kisha kuidondosha helkopta aliyokuwa akiiendesha wakati alipoungana na Askari wanyamapori waliokuwa wakikabiliana na majangili katika pori la akiba lililopo katika wilaya ya Meatu Mkoani Simiyu.

Watanzania watakiwa kushirikiana na China kwa ajili ya maendeleo

Waziri Mkuu mstaafu MIZENGO PINDA amewataka watanzania kutumia uhusiano uliopo kati ya TANZANIA na CHINA kujiletea maendeleo katika mambo mbalimbali hususan uchumi.

Waziri PINDA ameyasema hayo katika sherehe za kuukaribisha mwaka mpya wa KICHINA zilizofanyika jijini Dar Es Salaam na kusema ili kuwa na uchumi imara kama uchumi wa nchi ya CHINA ni lazima wananchi wawe na nidhamu ya kazi na kujituma kwa moyo mmoja.

Amewataka watanzania kutumia fursa ya ushirikiano baina ya CHINA na TANZANIA kwa kuiga ari ya ufanyaji kazi ili kuinua uchumi wa nchi.

Rais Magufuli aelezea kusikitishwa na Majangili Kumuua Rubani Rais wa Uingereza huko Meatu

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amelaani kitendo cha watu wanaosadikiwa kuwa ni majangili kumuua kwa kumpiga risasi Rubani wa helkopta Kepteni Roger Gower, raia wa Uingereza na kisha kuidondosha helkopta aliyokuwa akiiendesha wakati alipoungana na Askari wanyamapori waliokuwa wakikabiliana na majangili katika pori la akiba lililopo katika wilaya ya Meatu Mkoani Simiyu.

WAZIRI MKUU Majaliwa amtaka Nape kuandaa kikao cha haraka

WAZIRI MKUU AAGIZA KIKAO NA WAKUU WA VYAMA VYA MICHEZO

 

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemtaka Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kuandaa kikao cha haraka na viongozi wa vyama vya michezo nchini ili wamueleze kila mmoja amejipanga vipi kuinua viwango vya michezo katika chama chake.

 

Ametoa agizo hilo leo mchana (Jumamosi, Januari 30, 2016) wakati akizungumza na mamia ya viongozi na wakazi mbalimbali wa mkoa wa Dodoma ambao walishiriki mashindano ya mbio za nusu marathon (km. 21 na km. 5) zilizofanyika leo mjini Dodoma.

 

Rais Dkt. John Pombe Magufuli amefanya uteuzi wa Makatibu Tawala

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amefanya uteuzi wa Makatibu Tawala wawili wa mikoa ya Mwanza na Katavi ili kujaza nafasi za Makatibu Tawala wa mikoa hiyo.

Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue amesema Rais amemteua Kamishna wa Polisi, Clodwing Mtweve kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza, ambako anakwenda kujaza nafasi iliyoachwa wazi na Faisal Issa ambaye uteuzi wake ulitenguliwa.

Pages

Ad
Subscribe to Focus Media RSS