Home » Node

Mohammed Alloush anasema hana matumaini ya kupatikana kwa mwafaka

Mwakilishi wa upinzani katika mazungumzo ya amani ya Syria Mohammed Alloush anasema hana matumaini ya kupatikana kwa mwafaka baada ya mazungumzo hayo kuanza jana mjini Geneva nchini Uswizi.

Kiongozi huyo wa upinzani amesema kuwa haitawezekana wao kama wapinzani kuunda serikali ya umoja wa washirika wa karibu wa rais Bashar Al Assad.

Alloush, ameongeza kuwa haiwezi wao kuingia katika muunganano na watu ambao amewaalezea kuwa wanaendelea kuwauwa watoto wao.
Aidha, ameishtumu Urusi kwa kuendelea kumuunga mkono rais Assad na kuendeleza mashambulizi katika ngome zao.

Mahakama ya rufaa nchini Misri imebadilisha hukumu ya kunyonga Wafuasi wa Brotherhood

Mahakama ya rufaa nchini Misri imebadilisha hukumu ya Mahakama kuu nchini humo iliyotaka wafuasi 149 wa kundi lillopigwa marufuku la Muslim Brotherhood kunyongwa .

Mahakama imetaka watu hao kushtakiwa upya kwa tuhma za kusababisha mauaji ya maafisa wa polisi 13 karibu na jiji kuu Cairo mwaka 2013.
Watu wengine, 37 walikuwa wamehukumiwa kifo na Mahakama ya rufaa imewataka kujisalimisha ili kufunguliwa upya mashtaka yanayowakabili.

Francis Wambete ni Mchambuzi wa siasa za Kimataifa na Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Makerere jijini Kampala nchini Uganda.

 

Wabunge Uingereza kujadili mapendekezo ya Waziri Mkuu

Wabunge nchini Uingereza wameanza kujadili mapendekezo ya Waziri Mkuu wa nchi hiyo David Cameron kuhusu mabadiliko ambayo Uingereza inayataka katika Umoja wa Ulaya.

Akiwasilisha mapendekezo yake hivi leo, Cameron amewataka wabunge nchini humo kuunga mkono mapendekezo hayo amabyo yanataka ushiriakiano zaidi na kuangazia ni vipi Uingereza inaweza kunuifaika ndnai ya Umoja huo.

Aidha, Cameron amesema hajawahi kusema kuwa Uingereza haiwezi kufanikwia nje ya Umoja wa Ulaya.

Watu wawili wamejeruhiwa baada ya ndege ya Somalia kutokea mlipuko

Polisi nchini Somalia wamesema kuwa watu wawili wamejeruhiwa baada ya ndege waliyokuwa wanasafiria kushika moto, huku wengine zaidi ya hamsini wakiwa salama.

Maafisa wa usalama nchini humo wanasema ndege ya shirika linalofahamika kama Daallo Airlines, ililazimika kutua katika hali ya dharura punde baada ya rubani wa ndege hiyo Vladimir Vodopivec, mwenye umri wa miaka 64, kusikia kitu kama mlipuko wa bomu.

Mgonjwa wa ZIKA texas alijamiiana

Shirika la Afya Duniani WHO hii leo siku ya Jumatano limetoa wito kwa nchi za Ulaya kuratibu mpango maalum juu ya kuzuia kuenea kwa mbu wanaosadi kiwa kuwa waenezaji wakubwa wa virusi vya Zika kabla mdudu huyu hajaanza safari yake kuelekea bara hilo la Ulaya.

Afisa wa umoja wa ulaya, Zsuzsanna Jakab amezitaka nchi za Ulaya kuchukua hatua ya kudhibiti mbu, haraka iwezekanavyo ikiwa ni pamoja na kuwashiriki sha watu wote.

Mahakama ya kijeshi imeanza kusikiliza kesi ya Germain Katanga

Mahakama ya kijeshi mjini kinshasa huko jamhuri ya kidemokrasia ya Congo imeanza kusikiliza kesi inayomkabili  aliyekuwa kiongozi wa kundi la waasi la FRPI , Germain Katanga al maarufu Simba kufuatia mauaji yaliyotekelezwa na kundi lake mwaka 2003 kijijini Bogoro nchini DRC.

Katanga mwenye umri wa miaka 38, alikamatwa mwezi Machi kwa uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya ubinadamu, ikiwemo mauaji na unyang'anyi, na kwa kushiriki katika mashambulizi ya kijiji cha Bogoro Mashariki mwa DRC mnamo Februari 24, 2003.

Upinzani nchini Syria umetoa onyo

Upinzani nchini Syria umetoa onyo juu ya mashambulizi yanayotekelezwa na majeshi ya serikali katika jimbo la Allepo yatavuruga mazungumzo ya amani yanayoendelea geneva uswizi.

Onyo hilo limetolewa na wajumbe wa kamati ya majadiliano HNC ambayo siku ya jumamosi  ilituma jopo la watu 17 wakiwemo viongozi watatu wa waasi kushiriki mazungumzo ya geneva.

Salim al-Muslet,msemaji wa kamati ya upinzani HNC  alibainisha kuwa upinzani ulikuwa ukisubiri na kufuatilia maendeleo ya jimbo la Allepo na majimbo mengine ikiwa masharti ya kusimamishwa mashambulizi yangetekelezwa.

Pages

Ad
Subscribe to Focus Media RSS