Home » Node

60% ya mapato ya mifuko ya afya kuboresha huduma za afya

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ameagiza asilimia 60 ya mapato yanayopatikana katika mifuko ya afya kutumika kwa ajili ya kuboresha huduma za afya.

Waziri MWALIMU amesema hayo bungeni mjini Dodoma wakati akijibu swali la mbunge wa viti maalumu mkoa wa TABORA, MUNDE  TAMBWE aliyetaka kufahamu mpango wa serikali katika kuboresha huduma za afya kwenye mikoa ya Tabora, Katavi na Simiyu.

Rais wa Iran Hassan Rouhani taifa lake liko tayari kuurejesha ukurasa mpya

Rais wa Iran Hassan Rouhani amesema taifa lake liko tayari kuurejesha ukurasa mpya wa ushirikiano wa kidiplomasia na Ufaransa, na hii baada ya kufikiwa kwa makubaliano ya kihistoria ya kudhibiti mpango wa nyuklia wa Iran ili nchi hiyo iondolewe vikwazo ilivyowekewa na mataifa ya magharibi.

Rouhani amewasili Paris hapo jana jumatano akitokea mjini Roma, wakati hafla rasmi ya kumkaribisha imefanyika leo asubuhi ikulu ya Elysée.

Chama cha wananchi hakitoshirikia katika uchaguzi wa marudio

Chama cha wananchi kimesema hakitoshirikia katika uchaguzi wa marudio  wa Visiwani Zanzibar uliopangwa kufanyika tarehe 20 marchi ya mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari muda mchache baada ya kumalizika kwa kikao cha Dharura cha baraza kuu la uongozi la Taifa,jijini Dar es Salaam,

Kaimu mwenyekiti wa Taifa CUF,Bwana Twaha Taslima, amesema wamefikia uwamuzi huo kutokana na uchaguzi huo kuwa ni batili

Sweden kuwafurusha takriban wahamiaji 80, 000,

Sweden imesema kuwa imedhamiria kuutekeleza mpango wa kuwafurusha takriban wahamiaji 80, 000, na baadaye hatua itafuta maombi yaliyotolewa na wahamiaji kupewa hifadhi nchini humo, wizara ya mambo ya ndani nchini humoi imesema.

Kwenye mkutano na waandishi wa habari mjini Stokholm Waziri wa mambo ya ndani wa Sweden Anders Ygeman amesema mpango huo wa kuwarejesha nyumbani wahamiaji hao utachukua miaka kadhaa.

Rais amteua Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, amemteua Ndugu Julian Banzi RAPHAEL, kuwa Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania.

Taarifa ya Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue imeeleza kuwa uteuzi huo umeanzia tarehe 26 Januari, 2016.

Kabla ya uteuzi huu Ndugu Julian Banzi RAPHAEL alikuwa Katibu Mkuu, Wizara ya Biashara na Viwanda, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

Mgombea urais wa Marekani Donald Trump hatashiriki mjadala

Mgombea urais wa Marekani anayewania kuchaguliwa na chama chake cha Republican Donald Trump hatashiriki mjadala wa siku ya Alhamisi unaorusha kwa njia ya televisheni, hatua inayokuja siku nne tu kabla ya jimbo la Iowa kuanza mchakato wa uteuzi.

Trump anayewania kuteuliwa na chama chake, aliweka hadharani wazo lake la kujiondoa katika mjadala huo wakati wa kampeni jana Jumanne huko Iowa, ambapo alisema, kuwa bila shaka hatashiriki mjadala.

Pages

Ad
Subscribe to Focus Media RSS