Home » Node

Umoja wa Mataifa umetuma mialiko kwa ajili ya mazungumzo mapya ya amani nchini Syria

Umoja wa Mataifa umetuma mialiko kwa ajili ya mazungumzo mapya ya amani nchini Syria yatakayofanyika mjini Geneva Uswisi juma hili, huku wawakilishi wa upinzani wakijadili kuhusu kuhudhuria au la.

Mialiko imetolewa huku vikosi vya serikali kwa kusaidiwa na ndege za kivita za Urusi vikifanikiwa kuuteka mji wa waasi kusini mwa Syria , katika ushindi wao wa karibuni tangu Moscow ilipoanza kampeni ya mashambulizi ya anga mwezi Septemba mwaka jana.

Serikali mpya ya umoja wa kitaifa nchini Libya itapendekezwa ndani ya siku 10

Serikali mpya ya umoja wa kitaifa nchini Libya itapendekezwa ndani ya siku 10 afisa mmoja amesema jana Jumanne , baada ya bunge la serikali inayotambuliwa kimataifa kupinga ile ya awali, hatua ambayo ni pigo kubwa katika juhudi za amani.

Mataifa yenye nguvu yamezitaka pande hasimu nchini Libya kuunga mkono serikali ya Umoja wa kitaifa iliyoundwa juma lililopita chini ya upatanishi wa Umoja wa Mataifa , kwa lengo la kumaliza mkwamo wa kisiasa ambao umechochea kuibuka kwa makundi ya kijihadi.

Kiongozi wa mapinduzi wa Vijana Ahmed Duma kushitakiwa

Kiongozi wa vijana nchini Misri Amr Ali ambaye vuguvugu lake la April 6 liliongoza mapinduzi ya mwaka 2011 yaliyomwondosha madarakani rais Hosni Mubarak atasimama kizimbani leo Jumatano kwa uchochezi, afisa wa mahakama ameeleza.

Mwendesha mashataka wa umma, aliamua jana Jumanne kupeleka shauri la Ali, mratibu mkuu wa vuguvugu hilo ambaye alikamatwa mwezi Septemba mwaka jana, katika mahakama ya uhalifu.

Kuwekewa vikwazo kwa rais wa Sudani Kusin

Jopo la wataalam wa Umoja wa mataifa wamependekeza kuwekewa vikwazo kwa rais wa Sudani Kusin , kiongozi wa waasi na maafisa wengine wawili kwa kuhusika katika vita ya kikatili nchini humo, wanadiplomasia wamesema jana Jumanne.

Orodha ya majina manne imefikiswa kwenye baraza la Usalama la Umoja wa mataifa katika waraka wa siri wa nyongeza kwenye ripoti ya jopo hilo ambayo pia inapendekeza kuwekwa kwa vikwazo vya kuingiza silaha nchini Sudan Kusini.

UNESCO yafanya kongamano kujadili mpango wa maendeleo sekta ya Elimu

Katika kuhakikisha elimu ya Tanzania inakua yenye ubora zaidi, Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) limepanga kuisaidia Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi kuandaa Mpango wa Maendeleo katika Sekta ya Elimu (ESDP), mpango ambao umelenga kusaidia serikali ya Tanzania kutengeneza maudhui na mikakati ya kuendeleza elimu kwa upande wa Tanzania bara.

 

Wabunge kujadili hotuba ya rais kwa siku tatu

Kwa mujibu wa taarifa kutoka ofisi ya Bunge ni kwamba Kanuni ya 23 (1) (i) ya Kanuni za Bunge, toleo la Januari, 2016, Bunge litajadili Hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, aliyoitoa wakati wa ufunguzi rasmi wa Bunge jipya la Kumi na moja tarehe 20 Novemba, 2015 .

Mjadala kuhusu hotuba ya Mheshimiwa Rais unatarajiwa kufanyika kwa siku tatu kuanzia tarehe 26 hadi 28 Januari, 2016.

Baraza la Usalama La Umoja Wa Mataifa kukutana na Rais Nkurunziza

Wajumbe 15 wa Baraza la Usalama La Umoja Wa Mataifa wapo mjini BUJUMBURA nchini BURUNDI ambapo wanatarajia kukutana na Rais PIERRE NKURUNZIZA wa BURUNDI na kufanya mazungumzo nae kuhusu amani ya nchi hiyo.

Mamia ya waandamanaji wanaounga mkono utawala wa Rais NKURUNZIZA walijitokeza nje ya uwanja wa ndege kupinga ujio wa wajumbe wa baraza hilo.

Nchi ya BURUNDI imejikuta katika ghasia baada ya Rais NKURUNZIZA kutangaza nia yake ya kugombea urais kwa muhula wa tatu na hatimaye kutekeleza azma yake.

Pages

Ad
Subscribe to Focus Media RSS